Robert Kelly aka R.Kelly Amekamatwa tena huko Chicago

Mwanamuziki Robert Kelly (R. Kelly) amekamatwa tena na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono, amekamatiwa katika Jimbo la Chicago.

R. Kelly anatuhumiwa kwa makosa 13 yanayohusisha ukatili wa kingono dhidi ya Watoto
Hii ni mara ya 3 kwa R. Kelly kukamatwa, alikamatwa mara ya kwanza mwezi February kwa tuhuma za kuhusika na makosa 10 ya ngono.
Mwezi May alikamatwa tena na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela.
credit;MillardAyo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment