UTAFITI: Kelele za Bar zinasababisha upungufu wa nguvu za kiume

Kama wewe unaishi karibu na Bar au kumbi za starehe basi huenda ukapatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume pale unapokuwa faragha.
Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema kuwa utafiti unaonesha kelele zaidi ya viwango husababisha upungufu wa nguvu za kiume, mimba kuharibika na kuleta athari za akili na afya ya ubongo.

Akizungumza na wamiliki wa Bar, kumbi za starehe na sherehe kuhusu athari za kelele zilizo juu ya viwango vilivyoainishwa mwaka 2015. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Samuel Mafwenga, amesema tangu mwaka 2016 hadi 2019 wamepokea malalamiko 4,790 ambayo kati ya hayo 952 sawa na asilimia 20 ni ya kelele.
Mafwenga alisema tafiti zinaonesha kelele zina athari kwa watoto kiakili, kiafya na kwa wajawazito na wazee pia.
Tafiti zinaonesha kelele zikizidi zaidi ya viwango zina athari ya faragha, hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume na kuwanyima watu faragha,” alisema Mafwenga.
Alisema tangu Januari mwaka huu hadi sasa amepokea malalamiko 200 ya kelele jambo ambalo linahitaji elimu zaidi ya uelewa juu ya athari za kelele.
Kwa mwezi mmoja uliopita nimepokea malalamiko 100 ambayo naendelea kuyafanyia kazi, hivyo kelele ni kero na zina athari ndani ya jamii kiafya na kimazingira,” alisema Mafwenga.
Alisema ili kuondoa kero hiyo ndani ya jamii, ni vyema wamiliki wakatumia vifaa vya kupunguza kelele ili waweze kupima viwango vya kelele wanavyovizalisha.
Hata hivyo, Mafwenga alisema kelele hizo hazihusu nyumba za ibada kwakuwa ana imani ni walinda amani.
“Mambo ya kuzingatia katika kudhibiti ni muda wa kelele, ukaribu wa makazi ya watu, ukaribu wa ukanda wa kudhibiti kelele, kelele za kujirudia, vipindi au mfululizo na nyinginezo,” alisema Mafwenga.
Akitaja viwango vya kelele vinavyoruhusiwa vimegawanywa katika makundi ya kawaida, kelele zinazoendelea viwandani au karakana, kelele za mara moja eneo la ujenzi, kutangaza kwa kipaza sauti, kumbi za starehe, nyumba za ibada, magari, migodi na machimbo.
Chanzo: Gazeti Mtanzania
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.