Idadi ya watu waliofariki ajali ya moto mkoani Morogoro yafikia 100

Idadi ya watu waliofariki dunia kwa kuungua moto katika ajali ya kulipuka lori la mafuta Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Msamvu mjini Morogoro imeongezeka kutoka 99 hadi 100 hii ni baada ya majeruhi mmoja kufariki usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema leo kuwa kwa sasa wamebaki majeruhi 15 kati ya 47 waliopelekwa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Majeruhi 15 waliobakia wamelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
credit;Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment