Msanii Mbalamwezi kutoka kundi la 'The Mafik' afariki dunia

Mmoja wa wasanii wanaounda Kundi la The Mafik, ajulikanaye kama Mbalamwezi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Msanii mwenzake wanaounda kundi hilo Hamadai amethibitisha.


Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana ingawa inasemekeana kutokana na majeraha ambayo yanahisiwa kuwa amepigwa. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu kifo chake

Aidha, Mjomba wa Marehemu aliyejulikana kwa jina moja tu la Mzee Chifu amesema kifo cha Mbalamwezi kina utata. Amesema marafiki zake waliopeleka taarifa ya kifo walieleza kuwa walikuta mwili wa Mbalamwezi umetelekezwa ukiwa hauna nguo

Mwili wa Mbalamwezi umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.