Teknolojia mpya ya Gym imeingia Afrika Mashariki

Mtanzania Emma Lehner Lyayuka ambaye ni muanzilishi wa Body Street Gym, baada ya kuishi na kufanya shughuli zake nchini Ujerumani, ameamua kuja na teknolojia mpya kwa wafanyaji mazoezi ya kujenga mwili (Gym), Emma ameleta teknolojia mpya inayomuwezesha mtu kufanya mazoezi pasipo kubeba vyuma kwa kutumia vifaa maalum.


Teknolojia hiyo inafahamika kwa jina la (EMS Work Out) maarufu kwa nchi za ulaya na tumezoea kuwaona baadhi ya wachezaji kama Cristiano Ronaldo na wengine wengi wakiitumia, huduma hiyo imeanzia Munich Ujerumani na kwa Afrika Mashariki, Tanzania ndio nchi ya kwanza kutumia teknolojia hiyo.


credit:MillardAyo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.