Nandy kumuita Billnas Bro wake kwa washtua Mashabiki

Wimbo wa pamoja kati ya Nandy na Billnas umeondoa taswira ambayo ilikuwepo kwa mashabiki wengi, ambao walikuwa wakiamini kuwa wasanii hao ambao wamewahi kuwa wapenzi hawana maelewano.

Kupitia Instagram zao wamekuwa wakiweka picha kadhaa huku zikiambatana na maneno ambayo yamekuwa yakionesha uchokozi, huku mashabiki wengi wakitoa maoni yao kuonesha watu hao huenda wapo pamoja.
Mojawapo ya 'Post' ambayo imepata Komenti nyingi, imewekwa na Nandy akiwa na Billnas kisha kuandika "Eti tunafanana na bro wangu?????"
Katika komenti wengi wameonesha kupinga hilo huku wengine wakitumia lugha kali, kejeli na kuwadhihaki wawili hao huku wakiitaja mara kwa mara video yao ya pamoja ambayo iliwahi kuvuja.
"Bro tena Nandy kwa 'kiss' lile jamani tuoneeni huruma basi mnatuchanganya," aliandika shabiki.
"Nandy unajua kuvuruga watu," aliandika shabiki mwingine.
Kwa mujibu wa Nandy na Billnas wanasema kwa sasa ni marafiki wa kawaida na ukaribu ambao watu wanauona NI kwaajili ya kibiashara zaidi lakini mashabiki wengi hawakubaliani na hilo.
"AMKENI BWANA ....WAMERUDIANA," aliandika shabiki mwingine
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment