Picha la Billnass na Nandy bado linaendelea

Issue ya wasanii Billnass na nandy kudaiwa wamerudiana bado inaendelea, baada ya rapa huyo kufunguka mengine yaliyotokea wakati wanashoot video ya wimbo wao wa Bugana.


Rapa uyo amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital ambapo amesema, alikuwa hajaguswa na hisia za kutaka kumtamani na kurudiana tena na Nandy, wakati wanashoot video hiyo licha ya kujiachia sana wakiwa wanashikana viuno, mapaja na kukiss mdomoni.

Pia amesema hata wakati anashoot video na Dayna Nyange, zilitokea changamoto zake kama hizo na mambo hayo ni kawaida tu kwenye muziki.

Aidha Billnass ameeleza sifa zingine za Wanaume wa Kinondoni tofauti na zinazosemwa na baadhi ya watu.

"Watafutaji kuliko sehemu yoyote.  Kwa Dar es salaam Kinondoni ndiyo kuna watafutaji na duniani kote huwezi kumkosa mwanaume wa Kinondoni ni watafutaji, wasafiri na mabaharia" amesema Billnass.

Pia Billnass ameeleza maana ya 'a.k.a' ya jina lake kwa kusema Mafioso ni Mafia, kama ambavyo nimelilainisha, kisheria haikufanyi kuwa hivyo ila unaweza ukawa Mafioso/Mafia kwa vitu vyako ambavyo unavifanya na yeye ni Mafioso kwenye muziki wake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment