Sina Mpango wa Kufunga Ndoa- Wema

UMEMSIKIA staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu? Bidada ameamua zake kuweka wazi kuwa hataki tena ishu za kuolewa kwani ameona kama zinamletea mizinguo.


Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema amesema ameona kuolewa na kuwekwa ndani kunaweza kumrudisha nyuma na kushindwa kufanya mambo yake ya kimaendeleo.


“Siyo siri, nimshaghairi kabisa ishu za kuolewa kwa sasa. Kama hiyo bahati haikuwepo huko nyuma, basi imeshapita maana mchongo wa kufunga ndoa sasa hivi ni kurudishana nyuma tu bila sababu za msingi,” alisema Wema mwenye umri wa miaka 30 akisisitiza sasa hivi ana mipango mingi ya kufanya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment