Ukaribu wa Rayvanny na Lulu Wamuibua Fahyma

Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram habari iliyoshika kasi huko ni madai ya uhusiano kati ya mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mwanamuziki Rayvanny.


Tangu jana Jumanne Septemba 3, 2019 habari za wawili hao zimekuwa mjadala huku zikiwekwa video zinazowaonyesha wawili hao wakicheza wimbo ambao Rayvanny na Will Paul.Wakati mambo yakienda kasi kwenye Instagram, Fahyma mzazi mwenzake Rayvanny amesema madai hayo hayana ukweli wowote.

Amesema licha ya kushuhudia katika mitandao ya kijamii ana amini hakuna kinachoendelea kati ya Lulu na Rayvanny.“Hata mie nimeona kwenye mitandao ila najua hakuna ukweli na wala kitu kama hicho hakiwezi kutokea.”“Namjua mume wangu ananipenda na mie nampenda hakuna wa kuweza kumchukua kwenye mikono yangu nafahamu hilo,” amesema Fahyma."
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment