Kwa Sasa Wapenzi ambao hawajafunga ndoa wataruhusiwa kulala chumba kimoja Hotelini huko Saudi Arabia

Raia wa kigeni ambao ni Wapenzi ambao hawajaoana sasa wanaweza kulala chumba kimoja cha hoteli na Wanawake sasa wataruhusiwa kupanga vyumba vya hoteli peke yao


Hayo ni sehemu ya mabadiliko ya masharti ya kupata 'Visa' yaliyotangazwa hivi karibuni na Taifa hilo ambalo limekuwa likiendeshwa na Sheria za Kihafidhina za dini ya Kiislamu

Wapenzi hapo awali walitakiwa kutoa uthibitisho wa kuwa wameoana kabla ya kupata chumba cha hoteli lakini hayo yamebadilishwa kipindi hiki ambacho Saudi Arabia inajipanga kukuza Sekta ya Utalii

Hata hivyo, Kamishna wa Utalii na Urithi Nchini humo amesema "Raia wote wa nchi hiyo wanatakiwa kuonesha vitambulisho vya familia au uthibitisho wa mahusiano wakati wa kukodi vyumba vya hoteli.”

Aidha, Mabadiliko hayo yanaeleza kuwa watalii wanawake si lazima wavae ushungi lakini wanategemewa kuwa watavaa kwa kujistiri vizuri

Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa ikionekana kama nchi yenye masharti magumu zaidi duniani na sasa utawala wake unajaribu kuiondosha picha hiyo kwenye mitazamo ya watu, hususani wawekezaji na watalii wa kigeni
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment