Zembwela Aondoka EAST Radio Aungana na Kitenge Wasafi Fm

Uongozi wa Wasafi Media ni kama umeamua kuzidi kufanya kufuru baada ya kuja na sapraizi ya maana jana ilipoamua kutambulisha watangazaji wawili.

Mtangazaji wa kwanza alikuwa ni Hillary Daud ambaye aliungana na Maulid Kitenge katika kipindi cha usomaji magazeti majira ya asubuhi.


Jioni tena katika kipindi cha Sports Court, kupitia Wasafi FM, Mtangazaji George Ambangile naye alitambulishwa na atakuwa pia anasikika kwenye Sports Arena.

Usajili wa watangazaji hao umezidi kuwa gumzo haswa katika kitengo cha michezo kutokana na watangazaj maarufu kusajiliwa ndani ya kituo hicho.

Gumzo lilianza kutokana na usajili wa mwanzo ambapo Maulid Kitenge sambamba na mchambuzi maarufu Edo Kumbwembe walipotangazwa na kutambulishwa kwa bashasha Jumatatu ya wiki hii ambao waliambatana na Yusuph Mkule, Mwanaidi Suleiman na Ahmed Abdallah.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment