Jibu la Ommy Dimpoz kwa TID Baada ya Kuambiwa Ajui Kuimba

Msanii Ommy Dimpoz amesema hana uhakika na kile alichokipost msanii TID, baada ya kumuorodhesha katika oroddha ya wasanii watano wabovu wa Bongo Fleva ambapo TID  alimuweka Ommy Dimpoz nafasi ya pili.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Ommy Dimpoz amesema hana uhakika kama ni TID kama ndiyo alipost kweli  katika mtandao wa kijamii wa Twitter,

"Kwanza mimi sipo Twitter kwa sababu akaunti yangu watu waliidukua taKribani mwaka sasa ila naishughulikia kuirudisha, Pili nilitumiwa tu hiyo "list" lakini mwisho wa siku sina uhakika kama ni TID mwenyewe, hata kama yeye ni kaka yetu kila mtu ana maoni yake na mtazamo wake" amesema

"Mwisho wa siku tupo katika nchi ya huru kila mtu anaweza kujisikia kwa kile anachokifanya, nilichukulia kawaida tu ila kwangu mimi ukiniuliza kuhusu TID nitakwambia ni mmoja wa wasanii bora waliowahi kutokea kwenye BongoFleva" ameongeza

Aidha Ommy Dimpoz amewajibu waliombeza kwamba hajastahili kuchukua tuzo za AFRIMMA kama msanii bora wa kiume Afrika Mashariki kwa kusema, "Mimi niliwekwa katika category, nikaomba kura kwa sababu walioniweka waliona nastahili kwahiyo hizo zote nichangamoto tu kwangu hakuna jipya"
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.