Nancy Sumari aja na Kitabu kingine cha watoto kinaitwa HAKI

Ninayo furaha kubwa na ya kipekee kutangaza ujio wa kitabu changu cha pili cha watoto! Kitabu hiki, kinachoenda Kwa Jina la Haki, ni hadithi iliyotungwa kutokana na sheria ya haki za mtoto ya mwaka 2009, ili kuweza kuwasaidia watoto wa Tanzania kuzijua na kuzilinda haki zao.
Karibuni , pametokea ongezeko la vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa Haki za watoto kwa namna nyingi, ikiwemo mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, na mengine mengi yasiyofaa kwa maendeleo na ustawi wa watoto wetu.

Kwa kupitia kitabu hiki cha Haki, ninatarajia kumfundisha mtoto wa Tanzania, kuzijua, kuzitambua na kuzilinda Haki zake, na vilevile kuibua mjadala kati ya watoto, wazazi, walezi, jamii na taifa Kwa ujumla, kuhusu Haki za watoto na namna ambavyo kila mmoja wetu, Kwa nafasi yake, anaweza kubeba jukumu la kuzisimamia pamoja na kuwalinda watoto wetu, katika Tanzania tunayoitaka.


Nancy ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bongo5 na taasisi ya Jenga Hub ambayo inatoa mafunzo ya matumizi ya vifaa vya teknolojia pamoja na ujuzi wa computer programming kwa watoto wa miaka 7 mpaka 12, amesema masuala ya mrembo ameyaweka pembeni kwasasa na kujikita zaidi kutoa elimu kwa watoto kupitia vitabu.
Kitabu hicho ni kitabu chake cha pili kwaajili ya watoto, kwani kitabu kitabu chache cha kwanza ‘Nyota Yako’ kilizinduliwa March 19, 2013.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.