Samatta aweka rekodi hii ambayo haijawekwa na mchezaji yeyote wa Tanzania pia na klabu yake ya Genk

Mshambuliaji kinara wa klabu bingwa ya Ubelgiji KRC Genk na nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta, hatimaye amepachika goli dhidi ya vigogo wa England majogoo Liverpool jana usiku katika michuano ya UEFA.
Ikumbukwe KR Genk wanacheza na liverpool mchezo wa marudiano kwani mchezo wa kwanza Liverpool walishinda kwa jumla ya goli 4-1 ugenini ambapo walichezea katika uwanja wa Genk nchini Ubelgiji.
Goli hilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Samatta lakini pia mashabiki wa mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla kwani licha ya Victor Wanyama kutoka Kenya anayechezea katika klabu ya Tottenham kuwepo kwenye michuano hiyo maendeleo yake sio mazuri kwani anawekwa benchi sana hivyo Samatta ndio muwakilishi wa nchi za Afrika Mashariki.
Hata hivyo, matokeo ya mwisho ya mchezo huo wa Klabu Bingwa Ulaya yalikuwa mabaya kwa Genk kwa kulazwa kwa goli 2-1.
Samatta, aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona mpaka wavuni ambapo alifunga goli hilo katika dakika ya 40 ya mchezo.
Mshambuliaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Ulaya tayari ameshapachika magoli mawili katika mechi nne, lakini pia ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuifunga klabu ya Liverpool na sio Mtanzania tu bali kaweka rekodi kuwa Mchezaji wa kwanza kutoka klabu ya KR Genk kufunga goli katika uwanja wa Anfiel unaomilikiwa na Liverpool.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Liverpool, Samatta pia alipachika bao la kichwa ambalo hata hivyo lilikataliwa baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Liverpool kabla ya kupachika bao.
Goli la kwanza la Liverpool katika mchezo huo lilifungwa na Georginio Wijnaldum katika dakika ya 14 baada ya safu ya ulinzi ya Genk kufanya uzembe wa kuondosha krosi iliyochingwa na winga wa Liverpool James Milner.
more on Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment