Vijana wa Chadema waeleza sababu za kumchangia Mbowe “hatutaki mamluki kwenye chama chetu”

Mwanachama wa CHADEMA na alikuwa Mgombea Ubunge Jimbo la KWELA kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 Daniel Naftali. Akizungumza na vyombo vya habari leo makao makuu ya CHADEMA wakati wa zoezi aliloliratibu la kuhamasisha vijana wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini kumchukulia fomu ya kugombea uenyekiti kwa kipindi kingine tena mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe.

Naftali ameeleza kuwa zaidi ya watu elfu ishirini na nane (28000) wamesaini petition ya kuitikia wito wakumuomba mwenyekiti wa CHADEMA kuridhia kuendelea kukiongoza chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano inayoishia Nov 2024.
Pia ameeleza wanachama na wapenda mabadilko wamechangia zaidi ya kiasi cha Tsh Milioni 5 kwajili ya Kulipia FOMU ya uenyekiti ambayo thamani yake ni Tsh Mil 1.
Vijana hao wa Chadema waliojitokeza kwa wingi makao makuu ya CHADEMA yaliopo mitaa ya Ufipa jijini Dar – Es – Laam wameiambia Bongo5 kwamba wameamua kuunga mkono kampeni ya kumchukulia Mh Freeman Mbowe fomu kwani wamemtaja kama mtu mvumilivu, mweledi na mwenye maono ya kuwaongoza na kuwavuusha salama katila kipindi kingine cha miaka mitano.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Fredrick Justine na pamoja na Mwenyeliti wa Vijama Ukonga wameeleza kwamba katika kipindi hichi kumekuwa na wimbi kubwa la wanasiasa wanaohama hama vyama wamejiridhisha kwamba Mh Freeman Mbowe ni mtu sahihi kwanibali na changamoto alizopitia ikiwemo kukaa gerezani, kufyekewa mashamba yame, club yake kuvunjwa pamoja na mambo mengine mengi magumu aliyopitia bado amesimama mstari wa mbele kukiongoza chama hicho kikuu cha upinzni nchini Tanzania. Pia wamewaomba wanachama wengine nchini wanaoona wanaweza kukiongoza chama hicho wajitokeze kwani mbali na wao kumuomba Mh Mbowe agombee tena haimaaninishi atapita bila kupingwa bali atapigiwa kura huku wakijinasibu kuwa chama chao ndio kinaongoza katika mapambano ya DEMOKRASIA nchini.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.