Zitto Kabwe Aongelea Vifurushi Vipya vya NHIF Asema Gharama zake ni Hatari

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe,  amesema vifurushi vipya vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni hatari kwa afya ya Watanzania

Zitto amesema kesho chama chake kitatoa tamko kuonyesha hatari inayoikabili taifa.

Alisema ni aibu kwa serikali inayojiita ya wanyonge kuamua kufanya afya kuwa bidhaa inayouzwa dukani kama shati.

Zitto aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa ” vifurushi vipya vya bima ya afya ya Taifa (NHIF) ni hatari kwa afya ya Watanzania. Chama chetu @ ACT wazalendo kitatoa kauli kesho kuonyesha hatari inayoikabili Taifa. Ni aibu serikali inayojiita ya wanyonge kuamua kufanya afya kuwa bidhaa inayouzwa dukani kama shati,”Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.